TWCC Savings and Credit Cooperative (SACCOs)

Yaliojiri katika mkutano wa mwezi/breakfast meeting tar: 10/2/2017
Kati ya mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano wa mwezi uliofanyika juzi tar 10 Februari 2017,

ni pamoja na kuhuisha SACCOS ya TWCC ili kuweza kusaidia  upatikanaji wa mitaji kwa wanachama. Baraka za kuhuisha SACCOs ziliwekwa wakati wa mkutano Mkuu wa dharura uliofanyika mwaka Jana 2016 tar 9 mwezi Juni. Hivyo kwa sasa makubaliano ni kuharakisha upatikanaji wa mtaji ili kuweza kuhuisha SACCOs kabla ya Mkutano Mkuu wa Mwaka huu.

Mambo yatakayofanyika
1. Wanatafutwa waanzilishi 50  wa kwanza, ili kuweza kuhuisha na baadae wanachama wengine watapewa nafasi ya kujiunga pia.
2. Kiwango kwa wanaopenda kuwa waanzilishi ni 200,000, ikiwa  ni lengo la kufikia  kiasi cha mtaji wa kuanzia unaotakiwa

3. Kiasi hiki yaani 200,000 kitajadiliwa katika kikao cha SACCOs kitakachofanyika Ijumaa Februari 17, 2017

4. Wote ambao hawakuweza kushiriki mkutano lakini wanatamani kuwa waanzilishi wa Saccos hii wanakaribishwa.(Kwa maelezo zaidi wasiliana na ofisi)

5. Mambo mengine yatakayo jadiliwa ni pamoja na kiasi kitakachotolewa (200,000), hisa  pamoja na thamani ya hisa, kiingilio pamoja na suala zima  la uwekaji akiba pamoja gharama za uendeshaji wa SACCOs.

6.Mwisho wa kulipa ni alhamisi tar 16 mwezi huu. Na watakaokuwa wamelipa tu ndio watakaoruhusiwa kushiriki kikao cha ijumaa kuwakilisha wengine.

*Wanachama walio mikoani watakaokuwa wamechangia na kuwa kati ya waanzilishi watakuwa wanafahamishwa kila hatua  inavyoenda kwa kuwa sio rahisi kushiriki vikao vyote Dar es salaam. Baadae watafahamishwa namna ya kusaini kabla ya usajili kama watahitajika kufanya hivyo.

* Wote mnaombwa kulipa kupitia
Bank: CRDB
 A/C: 01J1029021100
 A/C Name: Tanzania women chamber of commerce
Branch: Azikiwe
Akaunti hii itakua ya muda wakati mchakato wa kufungua akaunti maalumu ya SACCOs ukiendelea.

Mwisho: Tumeunda group la waliojitokeza wote kuwa waanzilishi. Kama hukuwepo na unahitaji kuwa mmojawapo tupatie namba na jina tukuunge.