CIRCULAR/ZERO WASTE FASHION APPLICATION

CIRCULAR/ZERO WASTE FASHION APPLICATION

CIRCULAR/ZERO WASTE FASHION APPLICATIOJe, wewe ni mwanamke au kijana unayejishughulisha na ubunifu wa nguo na mavazi?Hii fursa ni yako

Chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwa kushirikiana GIZ Business Scouts for Development Program (BSfD) wameanzisha mradi wa kuboresha ujuzi wako wewe mwanamke na kijana mjasiriliamali uliepo katika tasnia nguo na ubunifu wa mavazi ya mitindo ili kufanya mabadiliko katika Uzalishaji wa bidhaa rafiki kwa mazingira, na zinazo punguza taka zitokanazo na Ubunifu wa Nguo, mavazi na Mitindo.

Lengo ni kufanya mabadiliko katika Uzalishaji wa bidhaa rafiki kwa mazingira na zilizo endelevu kwa wanawake na vijana ambao tayari wanajihusisha na shughuli zinazohusiana ushonaji wa nguo na ubunifu wa mavazi katika chini na kuwa na uzoefu wa angalau miaka 3 katika biashara yako.

Kupitia mradi huu utapata:

➡️Kujengewa uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye tija ili kushindana kitaifa na kimataifa.

➡️Fursa ya kubadilisha biashara yako kuwa bidhaa rafiki kwa mazingira na zilizo endelevu.

➡️Kuwakutanisha wabunifu wa ndani na wale wa kimataifa kuweza kubadilishana uzoefu

➡️Kuwawezesha wajasiriamali kutangaza bidhaa zao kupitia Tamasha la Nguo na Mitindo Tanzania.

➡️Kuwajengea uwezo wa kutafuta masoko na kuwaunganisha kidigitali

➡️Kuwaunganisha na majukwaa ya Mitindo Endelevu

Tuma maombi yako kabla ya tarehe 05 Novemba, 2023 kwa kujisajili kupitia www.twcc-tz.org
Au Pakua Fomu ya maombi na ujaze kupitia Link hii  JISAJILI HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *