AGRIBUSINESS DEALROOM

TWCC inakuletea karibu yako fursa za uwekezaji na mitaji kupitia Jukwaa la AGRIBUSINESS DEALROOM. Hili ni jukwaa maalumu kwa ajili ya kuwakutanisha wadau wote katika mnyororo wa Sekta ya kilimo kwa ajili ya Ubia na Uwekezaji.

Hivyo, AGRIBUSINESS DEALROOM imefungua dirisha la maombi kwa Wakulima na Makampuni/Wafanyabiashara wa bidhaa za Kilimo ambao wanahitaji Wabia (Partners) na Wawekezaji (Investors).

Watakaochaguliwa watanufaika na fursa zifuatazo;👇🏿

1. Kupata Mitaji (Access to finance/Capital)
2. Uangalizi maalumu (Mentorship)
3. Jinsi ya kuingia sokoni/ Fursa za masoko (market entry solutions)

SIFA ZA MUOMBAJI👇🏿
1. Kampuni au Biashara ni lazima iwe inahusiana (clear link) na Wakulima wadogo kama vile uuzaji wa pembejeo, umwagiliaji, usafirishaji, huduma za kifedha, uongezaji thamani, majukwaa ya kidigitali na kadhalika.
2. Mpango wa biashara ( Business Plan/Business Model)
3. Kuchochea maendeleo ya vijana na ujumuishi wa kijinsia
4. Rafiki wa mazingira
5. Uwezo wa kuvutia wawekezaji (Mazingira mazuri ya ushirikiano na uwekezaji)

Tuma maombi yako kupitia👇🏿

https://agribusinessdealroom.org/for-smes/ au jaza fomu iliyoambatanishwa katika ujumbe huu na utume kwa barua pepe👇🏿

dealroom@agra.org

Mwisho wa kutuma maombi ni 07 Mei, 2023.

Maelezo zaidi tupigie kupitia nambari za simu 0757 823 982

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *