DAR ES SALAAM INTERNATIONAL TRADE FAIR 2023

TWCC MAONYESHO YA SABASABA 2023 🔥🔥🔥🔥🇹🇿👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼
Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kinapenda kuwatangazia wanachama na wanawake wote wajasiriamali kutoka Mikoa yote kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki maonesho ya Sabasaba.
Tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2023
Gharama za ushiriki
1. Kibanda Cha Mita 9 wanakaa watu 4 (Kila mmoja )ni sh. 200,000 kwa washiriki kutoka nje ya Dar es salaam
2. Kibanda cha Mita 9 wanakaa watu 4 ( Kila mmoja) ni sh. 250,000 kwa washiriki kutoka Dar es salaam
3. Kibanda cha Mita 9 wanakaa 3 ( kila mmoja) ni Tsh. 300,000 kwa washiriki kutoka mikoa yote
4. Nusu kibanda ni Tsh. 400,000 ( Kila mmoja) kwa washiriki kutoka Mikoa yote (Nusu kibanda)
5. Kibanda kizima Mita 9 (Booth) – 800,000
Lipia Kupitia : CRDB Bank
Akaunti: 01J1029021100
Jina: Tanzania Women Chamber of Commerce
Gharama Zitahusisha;
Meza, Kiti🪑, Mapambo, Ulinzi,Umeme, Sare, Mafunzo, Matangazo
Mwisho wa kuthibitisha na Kulipia : 30 Mei 2023.
NB: Mshiriki atajigharamia kitambulisho. Gharama za Kitambulisho ni Tshs. 30,000/-
Kumbuka kujaza fomu ya ushiriki pale unapojiandikisha, ukitaja ukubwa wa eneo unalohitaji kulingana na bei hapo juu.
Bidhaa zinazoruhusiwa: Bidhaa kutoka sekta zote zinazozalishwa ndani ya nchi, pamoja na teknolojia ndogo ndogo za uongezaji thamani.
Kwa Mawasiliano zaidi ; tupigie kupitia namba:0757823982 au 0677070408