FASHION FOR CHANGE PHASE II – 2023

FASHION FOR CHANGE PHASE II – 2023

Fursa kwa washonaji wa nguo na wabunifu wa mavazi

Chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwa kushirikiana GIZ Business Scouts for Development Program (BSfD) wameanza utekelezaji wa Mradi mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali walio kwenye sekta ya Nguo na Ubunifu wa Mavazi awamu ya pili.

Mradi huu unalenga wanawake na vijana ambao tayari wanajihusisha na shughuli zinazohusiana ushonaji wa nguo na ubunifu wa mavazi katika nchi za Afrika ( Tanzania, Rwanda, Ethiopia na Uganda).

Hivyo wanawake na vijana wa kike walio katika sekta hii mnajulishwa kujiandikisha kushiriki katika programu hii kubwa ambayo ni endelevu.

Lengo la programu ni pamoja na;
1. Kuwawezesha wanawake katika sekta hii kuzitambua fursa kitaifa na kimataifa

2. Kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye tija ili kushindana kitaifa na kimataifa.

3. Kuwajengea uwezo wa kutafuta masoko na kuwaunganisha kidigitali

4. Kuwakutanisha wabunifu wa ndani na wale wa kimataifa kuweza kubadilishana uzoefu

5. Kuwapatia washiriki walezi (Mentors) kwa ajili ya kuwaongoza katika kuboresha bidhaa wanazozalisha

6. Kuwawezesha wajasiriamali kutangaza bidhaa zao kupitia Tamasha la Nguo na Mitindo Tanzania.

Ili kujisaji fungua link ifuatayo ujaze fomu kabla ya tarahe 20 Februari, 2023

au kujaza fomu inayopatikana Ofisi za TWCC katika Mikoa mbalimbali

Au

Bonyeza linki hapo chini kujisajili👇🏻
JISAJILI HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *