KONGAMANO KUBWA LA VIJANA
Je, wewe ni kijana mwenye umri kati ya miaka 15-25?
TWCC inapenda kuwajulisha vijana kuwa kutakuwa na kongamano kubwa la Vijana lililoandaliwa na Presidents Emergency Plan AIDS Relief (PEPFAR) kuhusu Afya litakalofanyika visiwani Zanzibar Tarehe 02 Oktoba 2024.
Kongamano hili limeandaliwa kwa ajili ya vijana ili kushiriki katika majadiliano ya kuboresha huduma za kinga na matibabu ya VVU kwa vijana.
Topic zitakuwa:
1. Jinsi ya kuboresha huduma za matibabu na namna ya kujikinga na HIV kwa vijana
2. Jinsi ya kuwawezesha na kuwashirikisha vijana katika programu za HIV
3. Jinsi ya kuimarisha huduma za kinga na matibabu ya HIV
Mwisho wa kutuma maombi ni 23 Agosti, 2024
N.B Kila mshiriki anatakiwa kujigharamikia usafiri kwenda Zanzibar
Kushiriki katika kongamano hili tafadhali bonyeza linki hii JISAJILI HAPA