TANZANIA & MALAWI BUSINESS FORUM

USHIRIKI WA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KWENYE KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA MALAWI NA TANZANIA (26-28 Aprili,2023)

TWCC inaratibu kupitia tawi lake la Mbeya.

Hivyo kwa wote wanaohitaji kushiriki gharama kutokea Mbeya jumla ya gharama ni shilingi 350,000/= ambayo itahusisha;

1. Nauli ya bus kwenda na kurudi hadi mji wa Mzuzu (Malawi) ambapo kongamano litafanyika
2. Gharama za malazi (3 nights)
3. Usafiri wa Ndani – Hotel kwenda kwenye Ukumbi

Aidha, Mshiriki anatakiwa kujiandaa na vifuaavyo,
1. Gharama za kupima Uviko -19 ambazo ni $ 100
2. Gharama za ziara akiwa kule – $ 100
3. Gharama za Chakula cha Usiku (dinner)

Washiriki wa kutokea mikoa mingine watasafiri hadi Mbeya ambapo wataungana na wenzao kwa ajili ya kuanza safari ya pamoja. Aidha, gharama za kutoka mkoa mwingine hadi mbeya hazijaunganishwa kwenye gharama za jumla za safari.

Malipo yafanyike kipitia;
Account number: 0133593281400
Jina: TZ WOMEN CHAMBER OF COM-MBEYA
Bank: CRDB

Deadline ya Malipo : 20/04/2023
Kwa mawasiliano zaidi:
0767197 222 ,0757823982

Faida za kushiriki kongamano ni pamoja na;
1. Kukutana na wafanyabiashara wa kutoka Nchi ya Malawi na kufahamiana na kujenga mtandao mkubwa wa kibiashara
2. Kutambua fursa zilizopo katika nchi ya malawi
3. Kukutana na wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kutoka Malawi
4. Fursa ya kutangaza bidhaa zinazozalishwa Tanzania kupitia maonesho yatakayoambatana na kongamano.

Wakati ni sasa, nchi imefunguka tutumie fursa vizuri.👌

Imetolewa na TWCC Makao Makuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *