Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme (TEEP) 2023

Tony Elumelu Foundation  Entrepreneurship Programme  (TEEP) 2023

TWCC inapenda kuwajulisha Wanachama wake kuwa
Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme (TEEP) 2023 imeanza usahili wa Vijana wenye mawazo ya biashara.
Mafunzo yatatolewa bure kwa vijana wajasiriamali kutoka Afrika na kuwapa mtaji wa Dola 5,000 ($5000).

WAHUSIKA
1.Vijana wenye mawazo ya biashara
2. Mmiliki wa biashara kuanzia mwaka 0 hadi miaka 5.

Waombaji wanatakiwa wawe vijana wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendeleza. Pia Muombaji anatakiwa awe na biashara moja tu.

MAFANIKIO
Watakaofanikiwa kuchaguliwa watapata fursa zifuatazo;-
1. Kupata mlezi (Mentorship)
2. Mafunzo kwa miezi 3 bure
3. Kujenga mtandao wa kibiashara
4. Mtaji wa biashara Dola 5000
5. Kutambua zaidi mtandao wa TEF
6. Kushiriki kongamano la TEF kila mwaka
7. Kuunganishwa na mtandao wa Wahitimu wa programu ya wajasiriamali wa TEF

Mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 31 Machi 2023
Tembelea link ifuatayo kwa ajili ya kujisajili JISAJILI HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *