TWCC YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE LA BAJETI

TWCC YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE LA BAJETI

Mapema leo tarehe 1 Juni, 2023 Uongozi wa TWCC Ukiongozwa na Mwenyekiti wa TWCC Taifa Mama Mercy Sila, Mkurugenzi Mtendaji Bi. Mwajuma Hamza na Mjumbe Wa Bodi Bi. Victoria Mwanukuzi wamekutana na Kamati ya Bunge ya Bajeti Bungeni, Dodoma na kuwasilisha mapendekezo ya kikodi ambayo ni changamto kwa wanawake wafanyabiashara nchini kwa ajili ya kuingizwa kwenye mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2023/2024.

Aidha, TWCC imewasilisha pia changamoto zinazowakabili wanawake wajasiriamali nchini zikiwemo za mazingira ya biashara pamoja na zinazohitaji mabadiliko ya sheria na sera mbalimbali.

 

 

Pia Uongozi wa TWCC uliambatana na Viongozi wa Vyama vya kisekta ambavyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wakandarasi (TWCA) Bi. Judith Odunga pamoja na katibu wa TWCA Bi. Debora, Katibu Wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini (TAWOMA) Bi. Salma Kundi, Mwakilishi wa Wanawake Wenye Viwanda Bi. Joyce Mmari kutoka Arusha pamoja na Mwenyekiti wa TWCC Mkoa wa Dodoma Bibi. Grace Oneya na Afisa Sera kutoka TWCC Ndugu. Godfrey Mondi.
Ni matumaini ya TWCC kuwa kamati itayafanyia kazi mapendezo tuliyotoa ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa Wanawake hapa nchini.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *